
“Nimekuwepo nje ya filamu kitambo nikiusoma mchezo, nimewaachie wasanii Chipukizi lakini bado aliyeonyeza uwezo hata kutufikia sisi wakongwe, jambo ambalo linanifanya nirudi tena katika fani, unajua zamani hadi muongozaji akukubali kuwa wewe unaweza ilikuwa shughuli, kwani ni lazima uwafunike wenzio wote waliopo katika kundi, lakini kwa sasa kuna wasanii wanapata bahati’” anasema Johari.
Anasema kuwa wasanii wengi wanaingia katika filamu hata kama uwezo wake ni wa kawaida kabisa na kazi zao zinapokelewa na jamii, anasema kuwa yeye hakuwa nje kabisa ya tasnia ya filamu bali alikuwa akiendelea na kazi ya filamu huku akiibua vipaji vipya kupitia kampuni ya RJ.







