
Langa, yeye mwenyewe anajikubali kuwa alikuwa teja lakini sasa anajitangaza kuwa amepona, hivyo ametangaza makamuzi kwa kwenda mbele.Ngoma iliyomrudisha Langa inakwenda kwa jina la ‘Kifo, Jela au Taasisi.’Ndani ya mzigo huo, kiitikio kinasema kuwa Kifo, Jela, Umma, Taasisi ndiyo mwisho wa uteja hilo halina ubishi.Katika wimbo huo, Langa anamaanisha kuwa mwisho wa teja yeyote ni kufa, kwenda jela, kuadhibiwa na umma au kuokolewa na taasisi zinazojihusisha na ukombozi wa vijana dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya.Langa anasikika ndani ya wimbo huo akisema: “Kila kitu kuhusu madawa ya kulevya aulizwe yeye kwa sababu ameshakuwa teja, akaonja chungu ya alosto na sasa ameacha poda (madawa).
“Hata siku moja teja hawezi kudumu ofisini, akikoswa na raia kaangukiwa na polisi. Nimekuwa teja miaka mitano nikapoteza potential, mama akaniambia nakuwa mento, ila sasa nina bomu kama Saddam ukiniwekea instrumental.”







