

Timu ya CPU ikijiandaa kupaa angani na Helkopita.
CPU Ni aina ya filamu ya kipelelezi yaani “Investigatory story” ikiwa inazungumzia kitengo kilichoundwa kwa ajili ya kufuatilia na kutatua matatizo mbali mbali wakati jukumu lao la kwanza ni kufuatilia juu ya mtoto mchanga aliyeokotwa pasipo kufahamika ni wa nani. Hivyo Maria Isabela (Sauda Simba) anateuliwa na serikali kuongoza timu hiyo, katika hilo inabidi awashawishi watakao msaidia ambao ni Alex Kibera(Nkwabi Juma) jambazi suguanayetumikia kifungo cha miaka 30 jela, David Kifati(steven Sandhu) mtaalamu wa kompyuta na kijana mwenye uelewa mkubwa ambaye anatoka katika familia bora na anayependa anasa.







