
Diamond ambaye hivi karibuni alimvalisha pete ya uchumba Wema ikiwa ni ishara kufungua ukarasa wa kuelekea kwenye ndoa, kwa sasa amebadilika.Site hii, ina SMS za Wema, akilalamika kuhusu mabadiliko ya Diamond, akieleza kuwa ana siku nyingi hajawasiliana na staa huyo wa nyimbo, Mbagala, Kamwambie, Nitarejea na Moyo Wangu.“Hapa nilipo nimechanganyikiwa, sijui itakuwaje. Diamond amebadilika, simuelewi kabisa,” alisema Wema na kuongeza: “Ananitesa sana, naumia sana.”Wema alisema: “Nina siku nne sijawasiliana na Diamond, nikimpigia simu hapokei, nikimtumia SMS hajibu. Hili ni tatizo kubwa kwa kweli.”
Hata hivyo, Wema hakusema walichotofautiana na Diamond, badala yake alisema: “Naogopa sana, kutokana na mambo ambayo yameshaandikwa kuhusu mimi, tutakapoachana itaonekana mimi ndiye mwenye matatizo.
“Tatizo langu na yeye silijui, ila nafahamu kuwa mama yangu hampendi Diamond, pia mama yake hanipendi na ameshawahi kunitamkia.”Diamond alipozungumza na ripota wetu, alikataa katakata kuzungumza chochote kuhusu ishu yake na Wema.







