"SUGU" - KUTOKANA NA MUINGILIANO WA RATIBA ANTI VIRUS KUZINDULIWA NOVEMBER 26
Posted on by Unknown
Anti Virus Volume II,Ambayo ilitarajiwa kuzinduliwa Novemba 5 mwaka huu kwenye Viwanja vya Posta,(Kijitonyama),Jijini Dar es Salaam.Taarifa mpya ni kuwa Anti Virus Volume II, itazinduliwa Novemba 26 Mwaka huu na hii ni kutokana na muingiliano wa ratiba.Habari zinasema kuwa Novemba 5 kwenye viwanja hivyo, kutakuwa na maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru.Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema kuwa kutokana na muingiliano huo wa ratiba, ilibidi vinega waambiwe wachague tarehe nyingine.“Baada ya kutafakari, tumechagua Novemba 26, ni siku nzuri. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza lakini ilibidi tuyapishe hayo maadhimisho,” alisema Sugu.