Upendo Nkone anatarajiwa kuwa miongoni mwa waimbaji watakaopamba tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mratibu wa tamasha hilo, Alex Msama wa Kampuni ya Msama Promotions, alisema Dar es Salaam jana kuwa Nkone amekuwa mwimbaji wa pili kuthibitisha kushiriki tamasha hilo baada ya Upendo Kilahiro. Tamasha hilo la aina yake, baada ya kufanyika Dar es Salaam, pia litarindima kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 9 mwaka huu. Tamasha la Pasaka mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.