Google PlusRSS FeedEmail

AFRICA MAGIC "HUU NI MWEZI WA KANUMBA"

Uamuzi ambao wameutoa Africa Magic Swahili baada kifo cha Steven Kanumba ni kwamba mwezi huu wote wa April wameamua kuuita MWEZI WA STEVEN KANUMBA ambapo wataonyesha movie zote za Kanumba kwa kipindi hicho.Africa Magic Swahili ni channel inayopatikana kwenye DSTV, Channel ambayo ni maalum kwa ajili ya kuonyesha movie za Kiswahili.
Afisa uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi amesema “Africa Magic wamefanya kazi kwa ukaribu sana na Kanumba, hata Africa Magic Swahili ilivyozinduliwa hapa Tanzania mwaka jana Kanumba alikua mmoja wa wasanii walioisupport sana, ni channel ambayo inatoa nafasi ya wasanii wa Tanzania kuweza kuuza movie zao na kuonekana Africa nzima” “Kanumba alikua asafiri Alhamisi kwenda Marekani kwa ajili ya kupromote movie yake mpya ambayo aliizindua na nasikia hiyo movie inafanya vizuri sana Ghana, tunatarajia kwamba kila kitu kikishakamilika baadae pia hiyo movie itarushwa kwenye channel ya Africa Magic Swahili”

KWA HISANI YA MILLAD

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging