Msanii wa maigizo ya filamu ELIZABETH MICHAEL mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa Tabata amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka tanayomkabili ya mauaji ya msanii mwenzake wa maigizo STEVEN CHARLES KANUMBA.
Wakili wa serikali Elizabeth Kagande alidai mbele ya hakimu Agustina Mbando kuwa mnamo tarehe 4 april mwaka huu eneo la Sinza mshitakiwa alimuua Steven Kanumba.Mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ya mauaji.Wakili alidai kwamba upelelezi haujakamilika na kesi hiyo itatajwa tena tarehe 23 mwezi wa nne mwaka huu.Mshtakiwa aliletwa mahakamani hapo kwa siri akiwa kwenye gari lenye namba za usajiri T848BNV aina ya Isuzu ambayo pia ilikuwa na Number nyingine za usajiri PT 2365 kwenye vioo.Mshtakiwa alisindikizwa na askari wawili wa kike na mmoja wa kiume....