Google PlusRSS FeedEmail

MAINDA NDANI MKE MWEMA AKIWA NA STEVE NYERERE

Mwigizaji  Ruth Suka ‘Mainda’ amesema kuwa baada ya filamu zake kadhaa kuingia sokoni na kufanya vizuri anatarajia kuingiza filamu mpya sokoni inayokwenda kwa jina la Mke mwema ambayo amefanikiwa kuirekodi hivi karibuni na kushirikisha wasanii wakali katika tasnia ya filamu hapa nchini. “Kwa mwaka huu nimepanga uwe wa kazi kwa kwenda mbele nimemalizia filamu mpya kabisa na ya kusisimua ya Mke mwema ambayo natarajia kuiingiza sokoni wakati wowote kuanzia sasa kwani kila kitu kipo poa ndio maana naweza kufanya chochote kwa ajili ya filamu hii,”anasema Mainda. Filamu hiyo ambayo imeigizwa katika mazingira ya kijamii tena maisha ya Kijijini  inaonyesha jinsi gani mke anavyoweza kujenga nyumba katika familia kama alivyofanya Mainda kwa kumrudisha mumewe na kuijali familia, filamu ya Mke mwema imeshirikisha wasanii kama Jengua, Steve Nyerere ambaye ni mumewe, Mainda mwenyewe, John Mafufu pamoja na wasanii wengine.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging