Google PlusRSS FeedEmail

NANI KUIBUKA NA TUZO WEEKEND HII KWA WAIMBAJI WA TANZANIA NA AFRIKA YA KUSINI?

Hapo kesho tarehe 28 tuzo maarufu za gospel nchini Kenya za Groove awards zinatarajiwa kutolewa huku mwimbaji Emmy Kosgei wa nchini humo akiwania kwenye vipengele vingi kwa upande wa waimbaji wa kike, kwa upande wa waimbaji wa kiume Juliani ndiye anaongoza kwa kutajwa kwenye vipengele vingi huku mwimbaji nyota Daddy Owen ambaye amekuwa akijizolea tuzo nyingi kila mwaka hadi kuamua kutoa tuzo yake ya mwimbaji bora wa kiume ya mwaka jana kwa Juliani,ambapo mwaka huu aliamua kutangaza kwamba hatakuwemo kwenye tuzo hizo licha ya kupendekezwa na watu kuanza kumpigia kura, akitoa sababu ya kutaka kuwapa nafasi waimbaji wengine. Katika tuzo hizo kuna category ya mwimbaji bora wa Tanzania tuzo ambayo ilichukuliwa na Christina Shusho mwaka jana huku Rose Muhando akishinda wimbo ulioongoza kwa upande wa watumiaji wa simu za mkononi ringtone.Mwaka huu waimbaji hao wamerudi tena kwenye kinyang'anyiro hicho akiwemo Bahati Bukuku,Neema Mwaipopo pamoja na mwanakaka Boniface Mwaitege huku likiwemo jina lingine la Neema Mushi ambalo bila shaka litakuwa limeingizwa kimakosa kwani mwimbaji ambaye alikuwa akilitumia jina la Mushi ni Neema ambaye kwasasa anaitwa Neema Mwaipopo au yawezekana kweli kuna mwimbaji mwingine aitwaye Neema Mushi.ila nani tuzo itamwangukia itajulikana jumamosi, pia tuzo hizo mwimbaji nyota wa kundi la Joyous Celebration Pastor Uche Agu ni mmoja wa waimbaji wakati wa utolewaji wa tuzo hizo pamoja na waimbaji wengine akiwemo Kambua.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging