Google PlusRSS FeedEmail

BEYONCE ADAIWA DOLA MIL.100



MWANAMUZIKI Beyonce amefunguliwa kesi ya madaia ya dola milioni 100 sawa na pauni milioni 62 na watengeneza video,baada ya kuvunja mkataba.Kwa mujibu wa mtandao wa digital Spy,madaia hayao yamefunguliwa na kampuni ya Gate Five ikidai kwamba nyota huyo alivunja makataba wa dola milioni 20 sawa na pauni milioni 12.5 walizokuwa wamekubaliana kutengeneza game ambayo ingepewa jina la Starpower: Beyoncé. Hata hivyo mwanasheria wa kinara huyo anadai kuwa alikuwa na haki ya kufanya hivyo kutokana na kuwa alifanya hivyo baada ya kubaini kwamba kampuni hiyo ya Gate Five,hawakukidhi kiwango cha bajeti ya kutengeneza gemu hiyo,ingwa waoa wanapigana na madaia hayo wakisema kuwa Beyonce hakufanya uungwana kwa kujiengua zikiwa zimebaki takribani siku tatu kabla ya kusaini mkataba na kampuni hiyo Desemba 2010.Kampuni hiyo inadai kuwa kitendo cha muimbaji huyo kiliifanya kampuni kupoteza mamilioni ya dola na kuwafukuza wafanyakazi 70.Gazeti la New York Post,liliripoti kwamba Jaji Charles Ramos,amesharuhusu kufunguliwa mashtaka hayo akisema kuwa Beyoncé,alipaswa kuwapa taarifa wamiliki wakampumni hiyo kabla ya kijiengua kwenye mkataba.Hata hivyo Beyonce, ambaye anaripotiwa kuwa na mpango wa kwenda London na mumewe Jay-Z na mtoto wao Blue Ivy, alikataa kuzungumza chochote kuhusu madai hayo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging