Google PlusRSS FeedEmail

LINEX SINGO YANGU NA DIAMOND HAIJAFANYA VIZURI

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Linex amekiri kwamba singo yake aliyofanya na Diamond haijapata mapokezi mazuri. Kwa mujibu wa mtandao wa Millardayo.com Linex alisema mapokezi ya single hiyo yalikuwa mazuri lakini si kama vile ilivyozoeleka anapotoa nyimbo zake.
"Mapokezi ya hiyo single yalikuwa powa lakini hayakuwa poa kivile kwa sababu kumbuka kwamba nilihama kwenye muziki, ule haukuwa muziki wangu, ile ilikuwa kwaito na watu wamenizoea kwenye muziki wangu kwa sababu wanajua Linex anafanya muziki wa hisia, nadhani hiyo ni moja ya sababu" alisema. Linex anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na na mchumba wake ambaye ni raia wa wa Finland alisema single hiyo haijamfikisha kule alipotaka kufika.Kwa hivi sasa ameachia single mpya inayoitwa 'Aiforaifora' "imefika point kwamba watu wakiwa kwenye mahusiano wakiachana basi moja kwa moja anakuwa akimlaumu tu mwenzake na hata kusahau vile vitu ambavyo alifanyiwa, nimezungumzia mwanamke au mwanaume mjinga ataivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe" alisema..

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging