Google PlusRSS FeedEmail

UTATA UMRI WA LULU WATUA MAHAKAMA KUU.

MAWAKILI wanaomtetea mwigizaji wa filamu Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji wamewasilisha Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam maombi ya uchunguzi wa umri wa mteja wao.Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidaiwa kutenda kosa hilo nyumbani kwa marehemu Machi 7 ,mwaka huu Mawakili hao waliwasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Mei 7 mwaka huu wakiomba iamuru kesi hiyo isikilizwe katika mahakama za watoto wakidai kuwa mteja wao ni mtoto Hata hivyo mawakili hao waligonga mwamba baadaya ya mahakama hiyo kutupilia mbali ombi hilo ikisema ingawa kesi bado iko katika hatua za awali haiwezi kufanya uchunguzi huo kwa kuwa haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo Jana mawakili wanaomtetea msanii huyo waliwasilisha maombi Mahakama kuu wakiiomba itoe uwamuzi kama mahakama ya kisutu inauwezo wa kuamua ifanyike uchunguzu wa umri halali wa msanii huyo kwa kuwa wanaamini kuwa ina mamlaka hayo Katika maombi hayo namba 46 mwaka 2012, yaliwasilishwa na wakili Peter Kitabatala kwa niaba ya jopo la mawakili hao pia wanaiomba mahakama Kuu kama itaridhika kuwa Mahakama ya Kisutu haina uwezo huo basi yenyewe ifanye uchunguzi huo. Akifafanua juu ya maombi hayo, Kibatala ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika( TLS), alisema sheria ya mtoto ya mwaka 2009, kifungu cha 113 inaruhusu Mahakama kufanya uchunguzi wa umri wa mshitakiwa Wakili Kibata alisema kuwa lengo la uchunguzu huo ni kuifanya ijiridhishe kama mshitakiwa ni mtoto au ni mtu mzima kwa lengo la kuangalia masilahi ya mtoto.Katika uamuzi wake, Hakimu Mkazi Augustina Mmbando anayesikiliza kesi hiyo alisema bado iko kwenye upelelezi na kwamba kulingana na jinsi ilivyo isingekuwa busara kuamua hoja yoyote na aliutaka upande wa utetezi uwasilishe maombi hayo kupitia Mahakama Kuu .Jopo la mawakili hao wanaomtetea msanii huyo linahitimishwa na Fulgence Massawe kutoka kituo cha Haki za Binadamu (LHRC). Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Mei 21 mwaka huu bado anaendelea kusota rumande kutokana na kesi inayomkabili kutokuwa na dhamana

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging