Muigizaji maarufu wa Filamu za kibongo Elizabeth Michael 'Lulu' alifikishwa katika Mahaka Kuu kuhusiana na kesi inayomkabili ya mauaji ya Bongo star Steven Kanumba. Utata wa umri wa lulu umeshindikana kupatiwa majibu kutoka mahakama ya Kisutu na kufikia mahakama Kuu mjadala ulidumu kwa mda wa masaa mawili na bado pia haukupatiwa majibu.Wakili Fungamtama ambaye ni moja kati ya wakili anayemtetea Lulu alidai mahakamani hapo kwamba kutokana na umri mdogo wa mtuhumiwa wanaiomba mahakama itoe udhuru kwa mtuhumiwa kushitakiwa katika mahakama ya watoto kwa kuwa ana umri chini ya miaka 18
Naye wakili wa serikali Elizabeth Kagandai alidai mahakamani hapo kuwa umri wa Lulu unatatanisha kutokana na maelezo yanayotofautiana na ya mtuhumiwa huyo aliyoyatoa awali kwani alipohojiwa na Jeshi la Polisi alidai kuwa na umri wa miaka 17, pia majina yake katika cheti cha kuzaliwa ni Diana Elizabeth tofauti na ilivyoandikwa kuwa ni Elizabeth Michael. Baada ya hoja kutolewa kesi hiyo imeahirishwa mpaka Juni 11 mwaka huu huku upelelezi juu ya umri sahihi wa lulu ili uweze kubainika....








