Google PlusRSS FeedEmail

WASANII WA FILAMU WAPO NYUMA- MH. MDEE.

Mbunge wa Kawe Mh Halima Mdee ameeleza kuwa wasanii wa filamu pamoja na kuwa na muonekano katika jamii lakini wapo nyuma sana katika masuala ya kijamii, lakini jambo baya kuliko yote ni kukosa umoja na ushirikiano katika masuala yao, hilo ameligundua katika kuugua kwa msanii mwenzao Juma Kilowoko ‘Sajuki’.“Wasanii wa filamu wapo nyuma sana kila mtu anajijali yeye tu hana msaada kwa mwenzake, leo hii Sajuki anaumwa na alikuwa akihitaji msaada wa kifedha ili akatibiwe nje ya Nchi lakini hakuna hata msanii mmoja aliyefanya juhudi zozote hata kuchangisha fedha hizo, tatizo lilomkuta Sajuki si tatizo la pekee yake mtu yoyote linaweza kumkuta,”anasema Mh. Mdee.Mbunge huyo mwenye mvuto Bungeni na mpiganaji katika masuala ya kijamii alitoa pongezi kwa kundi la Orijino Komedi kwa kubuni na kuvunja vipindi vyao na kutumia muda huo kuchangisha fedha kwa ajili ya kumsafirisha mgonjwa, pia anasema kuwa wao wanajitahidi kuibana Serikali Bungeni kuhusu maslahi yao na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo alitoa ahadi kuongelea maslahi ya wasanii katika bajeti mwezi wa saba.
Mh.Halima Mdee katika kuguswa na ugonjwa wa msanii Sajuki pamoja na kutoa fedha kwa ajili ya msanii huyo, pia aliungana na wasanii wa muziki sambamba na Waheshimiwa Wabunge katika kuimba wimbo maalumu kwa ajili ya kumchangia msanii Sajuki huku wasanii wa filamu wakiwa wachache ambao walikuwa ni William J. Mtitu, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Wema Sepetu na Wastara Juma pekee.Hali hiyo ambayo hata waheshimiwa wamaeanza kuiona ni tatizo, ni wazi wanawatetea watu walio katika makundi yasiyo na manufaa kwa wasanii wenyewe na jamii nzima kwa ujumla hivi sasa kuna kundi la TAFF na Bongo Movie Unity ni kundi gani linawakilisha maslahi ya wasanii wote kwa ujumla? Badilikeni ili muondoe taswira mbaya mliyojenga kwa jamii, hatuwezi kuwa maadui kwa kuongea ukweli...

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging