DIAMOND KUIMBA TAARAB
Baada ya kutamba kwa muda mrefu katika muziki wa kizazi kipya nchini msanii nyota wa muziki huo Naseeb Abdul ‘Diamond’ amesema anafikiria kujitosa katika muziki wa taarab.
Diamond alisema hayo jijini Dar es Salaam kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na kuvutiwa na muziki huo wa taarab, mshindi huyo wa tuzo mbalimbali za muziki amesema anajua uwamuzi wake huo utawashangaza mashabiki wake wengi , lakini ni jambo la kawaida kwa msanii
Diamond anasema hadi sasa anaamini hana mpinzani katika muziki wa kizazi kipya na hakuna msanii anayeweza kufikia kiwango chake hapa nchini
“Najua watu watanishanga na kuniona mtu wa ajabu, lakini nimefanya hivyo kwa sababu sina mpinzani katika muziki wa kizazi kipya” alisema
Anasema kuwa ameamua kupiga miondoko ya tofauti ya muziki kutokana na kipaji chake alichonacho katika fani hiyo ambayo imempatia umaarufu mkubwa, kutokana na kipaji chake hicho Diamond alisema kuwa hakuna kitu anachoshindwa kukifanya katika muziki
“Bado sijaanza rasmi kupiga muziki wa taaarabu ninachokifanya kwa sasa ni kufanya tathimini la soko lake ili kuona kama unaweza kuniletea mafanikio kama ilivyo kwa muziki wa bongo Fleva