Google PlusRSS FeedEmail

JPLUS AZIDI KUNGARA TASNIA YA FILAMU


Jimmy Mponda, maarufu kama Jimmy Master, ni moja ya majina ambayo wadau wengi wa filamu si geni kwao kulisikia.Kabla ya kuingia katika tasnia ya filamu, Jimmy anasema alianza sanaa kwa kujiusisha na sarakasi 1978 ambapo 1980 alijiunga na kikundi kilichojihusisha na sarakasi, ngoma pamoja na maigizo ya stejini.

Mnamo 1986 alianza kujihusisha na biashara na pia alianza kujiingiza katika mchezo wa mapigano pamoja na karate akiwa mjini Arusha (YMCA).Mwaka 1999 alitoka Moshi na kuja Dar es Salaam, ambako alikuja kuishi moja kwa moja na kuhamishia mipango yake.

Anasema, "Mpaka sasa mimi ni kati ya wakongwe katika tasnia ya filamu nchini. Nikiwa nimepitia baadhi ya mambo mengi tu, kwani uwepo wangu mpaka sasa si mchezo. Nimefanikiwa kubaki ambapo wengi sasa wameishapotea."Nyota yake ya kuanza kufanya kweli katika tasnia ya filamu ni baada ya kutoa filamu ya kwanza ya mapigano ambayo ni filamu ya kwanza kutengenezwa nchini.

Jimmy ama J Plus anazidi kueleza kuwa kizazi kipya cha filamu za ki-Bongo, kimepata kuelewa kuanzia filamu ya Girl Friend iliyozinduliwa kwa mara ya kwanza 2000.Anasema filamu iliyotoka 2000 iliwahusisha wasanii kadhaa wa muziki wa Bongofleva ambao ni Khalid Mohammed na Top In Dar
'TID'.

Na pia akiendelea kuwataja majina wasanii wengine kama Juma Mchopanga 'Jay Moe', Ambwene Yessaye 'Ay', Gwamaka Kaihula 'Gk'na wengineoJ. Plus anawataja wasanii wengine walioweza kufanya kweli kwenye anga za runinga kuwa ni Vyone Charles 'Monalisa' pamoja na Beatrice Mource 'Nina' pamoja na Bakari Makuka.

Anasema kwa sasa wadau wa tasnia ya filamu wamezidi kuona mabadiliko lukuki, tofauti kabisa na siku za nyuma, kwani mabadilikoyanazidi kujili kila uchwao.J Plus anazidi kufunguka kwa kusema kuwa,"Miaka ya nyuma filamu zilikuwa zikioneshwa katika kumbi za sinema tofauti kabisa na hali ya sasa, kwani kumbi nyingi zimeacha kuonesha."

Anazitaja filamu zilizowahi kutikisa ambapo anaitaja filamu ya kwanza inayoitwa 'Fimbo ya Mnyonge' pamoja na filamu zingine kama 'Harusi ya Mariam' na nyingine iliyopewa jina la 'Watoto na Haki'.Filamu hizo zilizotajwa hapo juu, zilitengenezwa na Shirika la Filamu Tanzania huku filamu ya 'Shamba kubwa' ikitengenezwa na baadhi ya wajasiriamali wa mkoani Tanga.

Wadau wa tasnia ya filamu wanaielezea Tanga kuwa ni mkoa uliotoa chimbuko la wasanii wa filamu nchini kama Mwalimu El Siagi na mtunzi mahiri wa riwaya nchini Amri Bawji.Jamaa huyu J Plus amepata 'kushaini' kabla ya mastaa kama Steven Kanumba, Vincent Kigosi 'Ray', 'Single Mtambalike' 'JB', Mahsen Awadh 'Cheni' na wengine.

Aliowazidi kete ni pamoja na Hissani Muya 'Tino', Issa Mussa 'Cloud' pamoja na Nurdin Mohammed 'Chekibudi'.J Plus anasema,"Baada ya kutoa filamu ya 'Shamba kubwa' ulitokea mlipuko wa Sinema nikaamua kuwa kimya ili kujipanga."

Baadaye kijana huyu alikuja na ujio mpya wa filamu ya 'Misuko Suko,' ambapo alitoa toleo la kwanza mpaka toleo la tatu katika ujio wake huo wa filamu ya 'Misiko Suko'.Katika toleo la kwanza la filamu ya 'Misuko Suko' J.Plus aliwashirikisha baadhi ya wasanii akiwemo Sebastian Mwanangulo.

"Katika sehemu zilizofuata katika filamu ya 'MisukoSuko' niliweza kucheza na watu wengine," anasema JPlus.Kwa sasa, JPlus ni mmiliki wa kampuni iitwayo Jimpowood C0 Ltd, Kampuni yenye maskani yake DDC Magomeni jijini Dar es Salaam, ikihusika na mambo kama ya kuhariri na udurufu filamu .

Katika ujio wake wasasa katika filamu iliyoingia sokoni hivi karibuni, filamu ya 'Doble Jay aliwatumia watoto pacha, Kenned na Kenneth Josephat Mshana wote wa Dar es Salaam.Jimmy Master anasema katika moja ya kitu ambacho hatakisahau ni ajali mbaya ya gari iliyomtokea mwaka 1999 akiwa Biharamuro,mkoani Kagera ambapo gari alilokuwemo lilipinduka mara nne.Lakini anasema Mungu alimuepusha na kifo katika ajali hiyo, hivyo anamshukuru sana
Mwenyezi Mungu.


This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging