Google PlusRSS FeedEmail

MAPACHA WATATU BADO WAPOKATIKA GEMU

 Josee Mara ambae ni kiongozi na mmiliki wa band ya MAPACHA WATATU amesema “Kalalaaliyekua mkurugenzi wa Mapacha tumeshaachana nae mazima kwa sababu ilikua ni mjadala wa mda mrefu, Tumeshamalizana nae na zile taratibu alizoziomba zimeshafanikiwa na tumeshafanya mikataba chini ya Advocate Okale”“Kikubwa sasa hivi tunaangalia tunafanya nini ili kuwapa nafasi wanamuziki tulio nao MAPACHA akiwemo Catherine, January na Kambi… yani kama Josee Mara aliimba rangi ya chunga na Jojina ndani ya FM ACADEMIA miaka miwili na ndio akaja kutoka kwenye dunia kigeugeu basi mi naamini January na Kambi tutawapa nafasi na maisha yataendelea” – Josee Mara
KUHUSU KUBADILI JINA BAADA YA PACHA WATATU KUONDOKA: “Hatuwezi kubadili jina kwa sababu ni Brand huyo watatu atakua ni msikilizaji na mtazamaji ambae atakua anaisupport Mapacha” – Josee Mara Josee Mara mtoto wa Kimara amekanusha stori kwamba chanzo cha kuondoka kwa Kalala ni ugomvi uliotokea kati yao wawili, mbali na kukanusha akaongeza kwamba “hizo ni fununu tu na sijawahi kugombana nae na ndio maana leo wanasema ni Kiso kesho wanasema ni Jose Kalala Junior ambae wiki mbili zilizopita kupitia alitangaza kwamba amesimama kufanya muziki kwa muda wa miezi miwili amefanya kazi na Mapacha watatu kwa miaka miwili ambapo taarifa za yeye kuacha kufanya kazi na band hiyo alizitoa kwa wenzake mwezi mmoja uliopita baada ya kumaliza kufanya moja kati ya show zao za usiku.

Kwenye hii album mpya ya Mapacha haitosikika sauti ya Kalala na pia hata kwenye single mpya waliyofanya Mapacha na kumshirikisha Ally Kiba, sauti ya Kalala haijasikika…….. na hiyo haimaanishi chochote kwamba Kalala na wenzake hawako kwenye uhusiano mzuri, bado wanaongea lakini kikazi ndio hawako pamoja. Kwa kumalizi, Josee Mara amesema siku zote unapozoea kukaa na mtu akiondoka lazima ujisikie huzuni lakini baada ya muda flani unasahau, hicho ndio kinachotokea kwa Mapacha sasa hivi baada ya Kalala kuondoka lakini haijawaathiri kwa njia yoyote ile kwenye uchumi

KWA MSAADA WA millardayo.com

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging