Google PlusRSS FeedEmail

OSTAZ JUMA - "KWA YOYOTE ANAYEMTAKA DOGO JANJA RUKSA"

Wiki mbili zilizopita msanii Dogo Janja alijitoa katika kundi la Tip Top Connection na kurudi kwao Arusha kwa basi, lakini sasa amerejea Dar es Salaam kwa ndege na kusaini mkataba na kundi la Watanashati linaloongozwa na Ostaz Juma.Lakini katika hali ya kushangaza, meneja wake mpya huyo tayari ametangaza kuwa yeyote ambaye yupo tayari kumchukua kijana huyo anaweza kufanya hivyo. Kauli ya Ostaz Juma imezua maswali.Dogo Janja alipokewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam .Mapokezi yake hata hivyo yameibua maswali kuhusiana na hatua ya wazazi wa kijana huyo kumwachia bila ya uangalizi maalum. "Unajua japokuwa watu wengi wamesema kuwa mimi nilikosea, lakini hawajui lolote. Ninayejua ni mimi mtendwa, wengi walikariri yaliyosemwa na Tip Top kuwa mimi nilikuwa mtoro, mkaidi," alisema Dogo Janja akiwa uwanjani hapo."Lakini mimi nasema kama kweli ningekuwa na vitendo hivyo wasingetokea watu wengine na kunifadhili."Japokuwa mkataba wa makubaliano ya ufadhili huo na kampuni ya Watanashati uko tayari Janja amesema bado hajasaini mkataba huo."Kuna watu wangu bado nawasubiri watakapouona huo mkataba na kuridhika nao basi kila kitu kitakwenda kama tulivyopanga, unajua lazima ujiridhishe kwanza na hiyo ndiyo mipango," alisema.Kuhusu shule, Dogo Janja, aliyekwama kuendelea na masomo ya Kidato cha Pili katika Sekondari ya Makongo, alisema ataendelea lakini katika shuke nyingine aliyoahidiwa na Ostaz Juma."Kuna mengi tumezungumza na kukubaliana kuwa katika suala la shule nitakuwa nikipelekwa kwa gari na nisome katika shule binafsi nzuri na pia niendelee na muziki," alisema."Mbali na muziki, sasa hivi nitakuwa naigiza na filamu pia pamoja na akina Kitale maana tuko nao kwenye kundi moja la Watanashati."

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging