Google PlusRSS FeedEmail

SALAMU KUTOKA KWA AFANDE SELE


Tamko langu kuhusiana na lugha zilizotolewa na 20% kuhusiana na show yetu ya Zanzibar Music Award."Tulialikwa kwenye Zanzibar Music Awards, na kabla ya kazi makubaliano yote ya kazi kwa mujibu wa mkataba yalifuatwa, makubaliano hayo yalihusisha sisi kujigharamia gharama zote za nauli na Malazi (accomodation).Tulifika Zanzibar salama, tulipokua Zanzibar twenty alitaka agharamiwe huduma zote ambazo ni nje ya mkataba wetu, nikamuomba na kumsihi sana Ndugu yangu aheshimu mkataba, asitafute matatizo kwani tayari mpaka wakati huu tuna kesi na Halmashauri ya Manispaa ya Moro ambayo kimsingi siku husika (nilishatolea ufafanuzi siku za nyuma).Lakini yeye alipingana na mimi, akanibishia na kunisukuma Mbele ya wageni na wenyeji wetu, wakiwemo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seiph Ali Idi, Waziri Seiph Khatibu.Walikuwepo waadishi wa habari wa siku Nyingi Akiwemo Abubakari Liongo na Mkurugenzi wa Zenji Fm ndugu Tua Saidi Tua.
Mimi Selemani Abdallah Juma Msindi sihusiki kwa namna yoyote, na tabia zisizo za kuridhisha zinazoonyeshwa na Ndugu yangu 20%, ambae nimekua nae nyumbani kwangu hata kabla ya Tuzo zake Tano (Kili Music Award) ambazo kazi hizo zote hizo kaandikia nyumbani kwangu siwezi kuwa na tatizo nae ni ndugu yangu kiimani na kikazi..Nimekua nikisisitiza nidhamu kwa Ndugu zangu wote toka enzi za Ghetto Boyz, Watupori na Mabwasha'Kingdom, ambao wengine hawafanyi sanaa, ila nipo nao kwenye Familia yetu kubwa hapa Tanzania. Nimesikitishwa na kitendo hicho. Siku zote nimekua mwenye kuhitaji suluhu kwa namna ya Amani.
Verry sorry kwa wote ambao mumefadhaika kwa hilo. Tuendelee kuwa pamoja na msisite kutoa ushauri wenu, maoni ili Game letu lisonge. MUNGU ATUBARIKI.

                                                      Asanteni sana.
                                Selemani Juma Abdallah Mutabhazi Msindi.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging