Kwa mara ya kwanza Tamasha la Sauti za Busara mwakani litawakutanisha wanamuziki wakongwe wenye uhasimu mkubwa kimuziki JB Mpiana na Werrason.Kwa mujibu wa mtandao wa Digital Congo waandaaji hao wameamua hivyo baada ya kuona muziki huo ni mmoja wa ladha zinazokubalika sana barani Afrika na hivyo kuamua kutanua wigo wa vionjo ili kuleta ladha kwenye tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwezi wa pili wa mwaka.“Extra Musica, JB Mpiana, Werrason, Fally Fally ni miongoni mwa wanamuziki ambao waandaaji wanatarajia kuwaita” umesema mtandao huo. Waandaaji wameonyeshwa kusikitishwa kwao na ushiriki mdogo wa wanamuziki kutoka Congo huku wakiwataja wanamuziki wachache kama Freddy Massamba, Samba Mapangala na Virunga and Super Mazembe kuwa ndio waliowahi kushiriki tangu kuanzishwa kwa Tamasha hilo, uliongeza mtandao huo.Waandaaji watapitia maombi na vikundi vyote kujua pamoja na mambo mengine kama muziki wanaopiga ni wa kiafrika, kama kazi ya msanii husika ni orijino ya kwake, umaarufu wa mwanamuziki au kundi kwa watanzania, pia wataangalia kama hawatahitaji pesa nyingi kulingana na bajeti ya waandaaji, kulingana na matakwa hayo na mengineyo tutajitahidi kuwaalika wanamuziki wote maarufu wa Kongo kama Extra Musica, Staff Benda Bilili, Konono No. 1, Kasai All Stars, musicians Fally Fally, Werra Son, JB Mpiana na wengineo ambao tunategemea wanamuziki na watanzania mbali ya kujifunza wataburudika pia,.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.