William Balfour ambaye aliyemuua mama,kaka,na binamu wa mwanamuziki Jennifer Hudson,amehukumiwa kifungo cha maisha jela..William Balfour alikutwa na hatia ya mauaji mwezi Mei..Jennifer Hudson ambaye pia ni mshindi wa Tunzo za Oscar alikuwepo wakati wa hukumu hiyo ikitolewa..wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo,waendesha mashitaka walidai kuwa William Balfour aliwauwa watu watatu wa familia moja baada ya dada wa Jennifer Hudson ambaye walikuwa wametengana nae na kukataa kurudiana nae..William Balfour amehukumiwa kifungo cha maisha jela kutokana na Jimbo la Illinois Kutoruhusu adhabu ya kifo..Hukumu hiyo imekuja baaya ya kesi hiyo kudumu takribani miaka mitano tangu kutokea kwa mauaji hayo mwaka 2008 na kusababisha vifo vya Darnell Donerson,Jason Hudson na mtoto wa miaka saba wa Julian...Jennifer Hudson alikuwa ndio shahidi wa kwanza kuitwa mbele ya mahakama kwa ajili ya kutoa ushahidi wake na alikuwa akihudhuria kila tarehe ya kesi ilipokuwa imetajwa,,,
Jennifer Hudson alikuwa akibubujikwa na machozi wakati William Balfour alipokuwa akisomewa hukumu yake
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.