Mara Baada ya kuanguka kwenye uchaguzi wa mwaka jana wa 2011 wa Wabunge, Mwanamuziki wa Zamani wa Wenge Musica BCBG Allain Mpela Afande amesema kuwa atarejea kwenye muziki kwa kasi. Mpela ambaye kwa sasa hana Albamu wala single yeyote inayo heat sokoni amesema kuwa anajikusanya ili atoe kitu kitakachotikisa anga la muziki.
Mpela amesema kuwa kwa sasa anaandaa Albamu yake ambayo itaitwa Flèche empoisonnée (Mshale wa Sumu) jina lainalofanya mashabiki kuwa na hamu ya kuisikia hiyo Albamu, Mpela ambaye ni kaka wa damu wa Mwanamuziki Geco Bouro Mpela ambaye aliwahi kuwa na Koffi Olomide aliyasema hayo kwenye Anniversary ya miaka mitano ya kifo cha Madilu System. Wote wawili waliondoka kwenye bendi zao na kujiunga kwa pamoja na kutoa albamu ya Mortal Combat ambayo haikufanya vizuri, wakiitolea maoni mtangazaji wa siku nyingi wa burudani Zakarie Bababaswe alisema kuwa kwa maoni yake Allain Mpella na Geco Mpella wote kwa pamoja waliwahi kuondoka kwenye bendi zao, bado walitakiwa kupata uzoefu zaidi