Google PlusRSS FeedEmail

STEVE NYERERE AGEUKIA SIASA




Muigizaji wa filamu na sauti ya viongozi mbalimbali nchini Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ amegeukia siasa ambapo jana amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC)

Steve Nyerere ambaye hivi karibuni aliipua Filamu ya mwalimu Nyerere ambaypo imezidi kumzolea umaarufu nchini, amesema ataendelea n asana yake ya uigizaji huku wakati akiwa NEC

Alisema amesukumwa kujiingiza kwenye siasa kwa kuwa yeye ni kada wa muda mrefu wa CCM hivyo kushawishika kuwania nafasio hiyo ili kuweza kukitumia vyema chama chake, msanii huyo alisema kama ilivyo kwa wasanii wenzake Asha Baraka ambaye ni Mkurugenzi wa African Stars Entertainment Tanzania (ASET) NA Khadija Kopa, ambaye ni muimbaji wa taarabu wanavyowawakilisha wanamuziki nay eye atatumia nafasi hiyo pia kuwawakilisha wasanii nchini, vijana na watanzania kwa ujumla

“Nilitumia sanaa yangu pamoja na jina langu kuzunguka nchi nzima kwa nia ya kuitangaza sanaa yangu na chama change hivyo wakati umefika kwa mimi kukitumikia chama” alisema

Aliongezea kuwa wadau na wapenzi wake wa filamu wataendelea kupata filamu zake kwa kuwa sanaa hiyo ipo ndani ya damu yake, hivyo hata kama ataendelea kujihusisha na siasa bado ataendelea kuwa msanii na mwakilishi wa wasanii wote

Msanii huyo amewataka watanzania kwa ujumla kumuunga mkono kazi zake na kila anachokifanya kwa kuwa anakifanya kwa mapenzi mema kwa mashabiki wake

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging