Google PlusRSS FeedEmail

WASANII WASHAULIWA KUWA WABUNIFU


Wasanii washauliwa kuwa wabunifu wa kazi zao ili kuufikisha muziki kwenye ngazi ya kimataifa na kuacha kunakili nyimbo hadi midundo isiyokuwa ya kwao .Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana katika Jukwaa la Sanaa ambalo huendeshwa na BASATA kila Jumatatu na mwanamuziki wa bendi ya The Kilimanjaro 'Wanjenje', John Kitime ambaye alikuwa mtoa mada.

Alisema kuna umuhimu wa kila msanii kufikilia kitu kipya na kama atakichukua cha mwenzi akifanyie maboresho ili apate cha kwake Kitime alieleza kuwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetakiwa kufuatilia kazi za wasanii wanaoshiriki kwenye tuzo za Kili Music, kwani baadhi ya wasanii wamekuwa wakituzwa kazi zisizo kuwa za kwao.

Akilizungumzia hatua hiyo, Kitime alisema baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakipewa tuzo wana tabia ya kunakili nyimbo zisizo kuwa za kwao na ndizo ambazo zimekuwa zikishindanishwa. Alisema kuna umuhimu kwa waandaaji wa tuzo hizo kwa kushirikiana na BASATA kufuatilia kwa karibu kazi za wasaanii hao, kabla ya kuwapa tuzo pamoja na kufuatilia kazi za wasanii waliopo mikoani.

Mwanamuziki huyo mkongwe alisema Tanzania kuna vituo vya redio 86 na zinazosikika hapa si zaidi ya 10 lakini wasanii ambao wamekuwa wakipewa tuzo ni waliopo Dar es Salaam. Kitime amesema kuna umuhimu wa kuziangalia upya tuzo zinazotolewa kwani waimbaji, ambao wamekuwa wakipewa tuzo hawaimbi muziki wa hapa nchini na badala yake wanapewa tuzo kwa kuimba nyimbo zenye asili ya mataifa mengine.

"Kuna umuhimu wa kuboresha tuzo za Kitanzania, ili kuitangaza na kukuza muziki kwa kuzivalisha tuzo hizi sura ya Tanzania," alisema Kitime. Alisema kuna umuhimu kwa BASATA kuanzisha bendi ya Taifa, ambayo inaweza kuwa mfano wa kuigwa na wanamuziki wengine.

Ametoa wito kwa serikari kuitupia jicho bajeti ya utamaduni na michezo, kwani kiasi cha fedha ambacho kimekuwa kikitolewa ni kidogo.





This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging