AUNT EZEKIEL KUFUNDWA MWEZI UJAO
Msanii mwenye jina na asiyeisha vituko, Aunt Ezekiel anatarajiwa kufundwa Oktoba 24, mwaka huu ikiwa ni maandalisi ya harusi yake inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni
Aunt Ezekiel ambaye kwa sasa inadaiwa hapikiki na wakwe zake , amekana hilo na kudai anapendwa kama 'Ubwabwa kwa njegere'na ndio maana atafundwa siku hiyo
'Shuhuli' ya kumfunda inatarajiwa kufanyika ndani ya Milimani City kabla ya wiki moja baadaye kufanyiwa sherehe katika hoteli ya Serena
Kuhusu kukataliwa ukweni, Aunt Ezekiel amedai taarifa hizo hazina ukweli wowote kwani anaamini watu wenye chuki zao ndio wanaosambaza uongo huo ili kumuharibia mambo yake
Alisema mpaka sasa taratibu za harusi yake zinaendelea kwa ushirikiano mkubwa wa wakwe zake na mume wake mtarajiwa aitwaye Demonte.
Haya yamekuja huku Aunt Ezekiel akiwa 'amechafuka' kutokana na picha zake za uchi kusambaa katika mitandao mbalimbali
Mwenyewe amekiri hilo na kudai kuwa wakati akifanya kitendo hiko alikuwa hajielewi kutokana na kuzidiwa na kilevi