Ni watu wachache mno ambao wanaweza kuamini kuwa unaweza kumkuta msomi mwenye digrii mbili akiamua kupanda jukwaani na kunengua kama mwanamuziki ,lakini hali hii ipo tofauti kwa mwanamuziki Koffi Olomide kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) pamoja na mafanikio aliyonayo kimuziki pia ni msomi aliyebobea katika maswala ya hisabati
Historia inaonyesha kuwa jina kamili la mwanamuziki huyo anaitwa Antoine Christophe Agbepa Mumba, alizaliwa mjini Kisangani mnamo Julai 13 1956
Kazi yake mwimbaji, mtayarishaji, na mtunzi wa muziki aina ya Soukous, inaelezwa kwamba baba yake ni raia wa DRC ambaye anatokea kwenye kabila la Gbandi ambalo linapatika katika mkoa wa Equateur ,wakati mama yake ni mzaliwa wa nchi hiyo pia akitokea katika kabila la Songye ambalo linapatikana katika mkoa wa Kasai na awali walikuwa wakiishi nchini Sierra Leone
Kwa mujibu wa mila nautamaduni wa kabila la babu zake mama yake alimpa jina la ‘Koffi’ kutokana kuwa alizaliwa siku ya ijumaa ,alijulikana katika mji mkuu huo wa Kinshasa akiwa katika familia ya watu wenye uwezo wa kati na mahali ambapo elimu ilikuwa ikipewa kipaumbele
Kwa mujibu wa historia hiyo, kijana huyo alikuwa anaakili darasani hali ambayo ilimfanya apate wadhamini wa kumlipia kwenda kusoma mjini Bordeaux, Ufaransa ambapo alipata shahada yake ya kwanza ya biashara na uchumi
Mbali na shahada hiyo inaeleza pia ana shahada ya pili katika masuala ya hisabati kutoka chuo kikuu cha paris
Akiwa Paris, alianza kujifunza kupiga gitaa na kuandika nyimbo na aliporudi DRC alijiunga na bendi ya muziki ya muziki ya Viva la Musica ambayo ilikuwa ikiongozwa na Papa Wemba ,baada ya kujiunga na bendi hiyo Koffi aliimarisha mtindo wa polepole wa soukous uliokuwa umeisha umaarufu
Aliuita mtindo huo Teha Tcho na ulipata umaarufu njee ya Kongo, akiwa katika bendi hiyo mwanzo alikuwa ni mtunzi wa nyimbo, mwandishi na baadaye kama muimbaji, na hata baadaye aliamua kujitenga na kundi hilo na kuanza kuimba kama mwanamuziki wa peke yake na hadi mwaka 1986 alipounda bendi yake aliyoipa jina la Quartier Latin,ambayo mwaka 2006 iliadhimisha jubilee ya miaka 20
Tangu kipindi hiko alikuwa akifanya kazi sehemu zote mbili aidha kwa kushirikiana na kundi hilo ama wakati mwingine peke yake hali hiyo ndiyo kwa miaka mingi imemjengea heshima mbele ya mashabiki wake kimataifa hususani Afrika na Ulaya
Yeye ameshiriki katika mradi wa muziki wa Salsa wa Africando, Koffi ameshinda tuzo nne za Kora Afrika na kusini na pia msanii bora katika Afrika ya Kati
Ameoa na anawatoto saba ,albamu ya Olomide Haut De Gamme KoweQt, Rive Gauche imeorodheshwa katika albamu 1001
Amewafundisha wanamuziki wengi chipukizi ambapo wengine wameamua kujitegemea na kusimama wenyewe katika kazi za muziki na wengine bado wapo na bendi hiyo hiyo
Baadhi ya wanamuziki ambao ameshawatoa ni Fele Mudogo, Sam Tshintu, Suzuki 4*4, Fally Ipupa, Ferre Gola
Hata hivyo katika siku za hivi karibuni Suzuki amekuwa akionekana mara kwa mara katika maonyesho ya Quartier Latin sambamba na mwanamuziki wa kike mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni Cindy Le Coeur