BAADHI YA 'MAPRODUCER' NCHINI WANACHORA
IMEELEZWA kuwa sababu zinazosababisha kufanana kwa kazi za muziki hususani wa kizazi kipya ni kuitokana na maproducer kushindwa kupiga kinanda 'live' na matokeo yake wanachora mtindo wa midundo wanayoitaka kwa kutumia komputar
Hayo yalielezwa na Producer anayekuja kwa kasi kwa kutengeneza nyimbo zinazofanya vizuri Afrika Mashariki Emanuel Maungu 'E.M.A theboy' alipokuwa akielezea sababu zinazosababishwa kuwa na mfanano wa kazi za muziki wa bongofleva
Alisema tatizo liko kwa maproducer ambao ni wavivu wasiotaka kubadilika na kusoma muziki hivyo wanashindwa kutumia vifaa ili kutengeneza muziki ulio na ubora zaidi
Alileza kuwa tatizo la kuwa na kufanana kwa kazi hiyo inatokana na maproducer kushindwa kutumia kinanda hivyo wanategemea komputar pekee kutengeneza muziki wakati wanatakiwa kujua kupiga kinanda 'live' alafu ndio utengeneze muziki kwenye komputar
"Tatizo maproducer wengi wanachora sababu ambayo inachangia kupata muziki unaofanana na kukosa ladha ya muziki kwani kwa kutojua kinanda huwezi kupiga vitu vingi, pia inachangia kutumia muda mrefu kutengeneza muziki" alisema E.M.A theboy
Mbali na hayo pia aliongezea kuwa baadhi ya wasanii pia hawajui kuimba na hawataki kujifunza hivyo matokeo yake kila siku kinaimba kitu kile kile na kupoteza ladha kabisa ya muziki wa bongofleva
E.M.A theboy ni producer amabye teyari ameshatengeneza nyimbo zinazofanya vizuri katika sekta ya muziki huu wa bongofleva nyimbo kama 'Sory' aliyoimba Barnaba, Upepo iliyoimbwa na Recho, 'Me anda you' iliyoimbwa na Ommy Dimpozi








