KILICHOTUMWA NA MARTN KADINDA KWENYE FACEBOOK
HUENDA mbunifu wa mavazi ya kiume Tanzania Martn Kadinda akawa baba mzuri hapo baadaye kwa kuonekana anauwezo mzuri wa kumbeba mtoto
Hali hiyo imeonekana baada ya Kadinda kupost picha kwenye mtandao wa kijamii facebook inayomuonyesha akiwa amembeba mtoto wa msanii wa kike Riyama Ally huku baadhi ya watu wakipost kwa kumpongeza kuwa na uwezo mzuri wa kumbeba mtoto tofauti na baadhi ya wanaume wengine
Kadinda amepost picha hiyo kwenye facebook huku akiwa ameandika maneno haya "instaMothers in Town.... #OneOfMyFavoriteActressInTanzania #RiyamaAlly #Fatma #cute"
Baadhi ya post zilizotumwa zilikuwa zinaonyesha kumpongeza mwanamama huyo kwa kupata mtoto wa kike pia kwa kuwa na nidhamu nzuri tofauti na baadhi ya wasanii wengine wenye majina makubwa katika tasnia hiyo ya filamu
"Nampongeza sana Riyama kwa kumpata mtoto mzuri na kuwa na nidhamu nzuri, kwani anajiheshimu kwenye jamii pia anajitambua" moja ya comment ilieleza hivyo
Riyama ni muigizaji wa siku nyingi amabaye pia anafanya vizuri katika tasnia ya filamu huku jina lake likibaki kuwa na heshima kubwa kwenye jamii yetu kutokana na nidhamu aliyonayo mwanamama huyo








