Google PlusRSS FeedEmail

BOB JUNIOR AELEZEA SABABU ZA KUOA MAPEMA




BAADA ya kuuwaga ukapela msanii na mtayarishaji wa muziki wa bongofleva Bob Junior 'Sharobaro'afunguka sababu zilizomfanya kuoa mapema, ikiwa moja ya sababu hiyo ni kuepuka kukaa kijiweni na kupunguza marafiki wabaya kwake

Akizungumza na safu hii Bob Junior alisema ameamua kuoa mapema ili aweze kujenga maisha yake na pia kupunguza marafiki wasio na umuhimu wowote kwani sasa mke wake ndio rafiki na mshauri wake

Alisema kabla hajaoa alikuwa anaishi maisha ambayo ni hatarishi ya kushinda vijiweni na kuwa na marafiki rukuki ambao walikuwa ni hatarishi kwa maisha yake

"Unajua bwana kabla sijaoa nilikuwa naishi tu vishawishi vingi ila sasa nimeamua kuoa na kutulia na mke wangu, kikubwa ni kuwa tunaheshimiana na kusikilizana" alisema Bob Junior

Alisema mbali na hayo pia ameoa mapema kwa sababu yeye ni mtoto wa kislamu na amelelewa katika maadili ya dini hivyo sheria ya dini inamruhusu mwanaume kuoa pindi tu anapobalehe

Alitoa ushauri kwa baadhi ya vijana wenzia ambao bado hajaoa na wanauwezo wa kuoa wafanye hivyo na wasiingie na uoga wa kuamua kuoa

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging