Picha ya (kushoto) inaonyesha Jamie Foxx akiwa na mtoto wake miaka 8 iliyopita na picha ya( kulia) ni ya wakati huu alipoudhuria tuzo hizo kwa mwaka huu
Baada ya miaka 8 kupita toka Jamie Foxx atokezee na binti yake katika tuzo za Oscar mwaka 2005, staa huyo alitinga tena na binti yake katika tuzo hizo siku ya Jumapili. Mwaka 2005, Foxx alishinda tuzo ya Oscar na alipanda katika jukwaa lenye kapeti jekundu akiongozana binti yake Corinne wakati huo binti huyo akiwa na miaka 11.
"Kuna mtu aliniuliza kama nilikuwa na wasiwasi kuhusu tuzo za Oscar. Nilimwambia, sina wasiwasi tena. Nina furaha ya kuwaonesha ni namna gani binti yangu amekuwa mzuri." Alisema Foxx siku ya Jumapili
Foxx,45, alisema kuwa alikuwa akiongea na binti yake, ambaye kwa sasa ana miaka 19 kuhusiana na maisha ya chuo na mapenzi wakati wako katika safari ya kuelekea katika sherehe ya tuzo hizo.