MRITHI WA SHAROMILIONEA APATIKANA
HATIMAYE ametokea mrithi wa marehemu Sharomilionea ambaye anaimba muziki na kuigiza miondoko yote iliyokuwa ikifanya na marehemu huku akiwa ameongeza vionjo vingine ili kuweza kuwateka mashabiki wake
Mrithi huyo anayejulikana kwa jina la Ramadhani Mohamed ambapo jina la kisanii anajulikana Sharomaburudani, akizungumza na Spoti Majira alisema kuwa kutokana na kufanana na marehemu Sharomilionea baadhi ya watu walimshauri kufanya kazi ambazo zilikuwa zinafanywa na marehemu
Alisema kuwa mbali na kufanana kwa miondoko ya kutembea na swaga pia anafanya muziki na sanaa ya vichekesho kwa kutumia mitindo ya marehemu ingawa amejalibu kuwa mbunifu kwa kuongeza vionjo vidogo mwishoni ambavyo vitaongeza radha zaidi
"Mimi nafanya kila kitu kama yeye ingawa nimejaribu kuongeza vitu vingine vyenye swaga za tofauti tofauti na ninatumia zaidi swaga za 'Black America'kuanzia mavazi hadi kuongea " alisema Sharomaburudani
Aliongezea kuwa ili kuthibitisha kuwa anauwezo wa kumrithi marehemu Sharomilionea hivi karibuni atatoa single yake inayokwenda kwa jina la 'darasa' ambayo imefanywa chini ya studio ya Wajukuu iliyopo Mbagara jijini Dar es Salaam
Alitoa wito kwa wadau na mashabiki wa sanaa kiujumla hususani muziki kutoa ushirikiano kwenye sekta hiyo ili kufikisha muziki wa bongo fleva katika hadhi ya kimataifa








