HALI YA MZEE SMALL YAENDELEA KUTENGAMAA
HALI ya msanii wa maigizo nchini mzee Small yaendelea kutengamaa siku hadi siku, huku akiendelea kuhudhuria mazoezi aliyopangiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kila siku
Hayo yalizungumzwa na rais wa Shilikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simony Mwakifamba jijini Dar es Salaam alisema kuwa anawashukuru watanzania wote kwa maombi yao na kuwa karibu na familia ya filamupindi matatizo yanapotokea
Alisema kuwa anashukuru pia hali ya mzee Small kuendelea vizuri siku hadi siku huku akiendelea kuudhuria mazoezi aliyopangiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na matibabu
"Tunamshukuru mungu kwa sasa Mzee Small anaendelea vizuri amesharuhusiwa hospitali ingawa bado anaendelea kuhudhuria mazoezi aliyopangiwa na kuendelea na tiba za kila siku" alisema Mwakifamba
Mbali na hayo aliongezea kwa kuelezea hali ya msanii wa vichekesho Matumaini kuwa inaendelea vizuri na inazidi kuimalika siku hadi siku na sasa yuko chini ya uangalizi wa wazazi wake nyumbani kwao
"Matumaini pia nayeye anaendelea vizuri kwa sasa na yupo nyumbani kwani amesharuhusiwa hospitali ingawa bado anaendelea kwa matibabu ya kawaida ila afya yake izidi kutengamaa" alisema Mwakifamba