Google PlusRSS FeedEmail

JACKLINE PENTZEL AWAKANA WAVAA VIMINI BAADA YA NDOABAADA ya kufunga ndoa na kubadilisha dini hivi karibuni  kimya kimya movie 'star 'wa bongo asiyekauka vituko' Jackline Pentzel a.k.a Jack wa Chuzi ameibuka na kuweka wazi kuwa hatoendelea kuvaa nguo zitakazo muonyesha sehemu kubwa ya maungo yake na badala yake kuanza kuvaa nguo za kumstiri

Akizungumza jijini Dar es Salaam Jackline alisema kuwa baada ya kufunga ndoa pamoja na  kubadilisha dini na kuamua kuwa muislamu  anaamini ndio muda wa kubadilika kwa kufuata maadili ya dini inavyotaka ikiwemo  kuvaa mavazi ya heshima

Kutokana na hali hiyo na kufanya uamuzi wa kubadilisha dini kwa ajili ya kumfuata mumewake ambaye anajulikana kwa jina la Gadner Dibibi msanii huyo aliweka wazi kuwa ameachana kabisa na mavazi mafupi pamoja na kuyaanika matiti yake hadharani huku akionyesha hali ya kusikitika kwa kufanya kitendo hiko hapo awali

"Kwa sasa siwezi tena kuvaa kama nilivyokuwa hapo mwanzo kwa sababu mimi ni mke wa mtu teyari na ninahitajika kufuata maadili ya mume wangu hivyo kwa sasa ni mwendo wa kuonekana nimevaa mabaibui pamoja na kujifunika muda wote" aliongezea kuwa

"Nimeamua kubadilisha dini kwa sababu mumewangu ni muislamu hivyo nimeamua kumfuata yeye kwa sababu ya upendo uliojengwa siku nyingi na mumewangu huyo" alisema Pentzel

Akizungumzia sababu iliyomsababisha kufunga ndoa yake kimya kimya alisema kuwa hakutaka kutangaza harusi yake kwa kuhofia maneno ya watu ambayo yangeweza kumbadilisha mawazo mumewake kitu ambacho yeye hakutaka kitokee

Alisema kuwa kutokana na kuwa mahusiano ya muda mrefu na mumewake huyo hatua iliyopelekea kuishi pamoja bila ya kufunga ndoa ndio sababu nyingine iliyosababisha wafunge ndoa hiyo kimaya kimya ingawa sasa wapo katika maandalizi ya kufanya sherehe ya kujipongeza baada ya kufunga ndoa hiyo

This entry was posted in

Leave a Reply

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging