KANYE WEST AMPIGA MKWARA KIM
Kutokana na hali ya ujauzito wa Kim Kardashiana, rapa Kanye West hataki kumuona mke wake huyo akipiga picha za utupu kwenye kipindi hiki ambapo wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza julai mwaka huu
Kim inasemekana anatarajiwa kutoka kwenye picha za jarida la Vanity Fair ambalo linamilikiwa na Demi Moore,lakini Kanye hataki kusikia hilo
"Ni kitu ambacho Kim amekuwa akitaka kukifanya kwa miaka mingi sana Anadhani litakuwa ni jambo zuri kitu ambacho kitaacha kumbukumbu milele" kilisema chanzo cha habari