LINDSAY KUENDELEA KUFANYA KAZI NA WAKILI WAKE
Kutokana na mwanasheria wa muigizaji mwenye utata nchini Marekani Lindsay Lohan kushindwa kutokea mahakamani wiki iliyopita muigizaji huyo hatamfukuza wakili wake
Hivi karibuni Heller alisaini mkataba wa kumwakilisha Lohan katika mashtaka yake ya kuvunja masharti ya kuwa chini ya uanagalizi kuhusu kesi ya wizi wa cheni ya dhahabu baada ya kuwaongopea tena poli kwenye ajali ya gari aliyoipata mwaka jana
Machi mosi mwaka huu Jaji wa Mahakama ya jiji la Los Angeles, Jim Dabney alimtimua Heller kwenye chumba cha Mahakama baada ya kuwasilisha hati zisizo sahihi, huku akimuagiza Lohan aidha kutokea mwenyewe mahakamani au kuthibitisha kama bado anataka Heller kuendelea kumwakilisha