TYRA BANKS AZIDI KUJITOLEA KWA WANAWAKE
Mwanamitindo Tyra Banks ametajwa kuwa ni miongoni wa wanawake wanaojitolea kwa ajili ya wenzao nchini Marekani, ingawa ni miongoni mwa wanawake wasiotulia kwenye mahusiano
Tyra Banks ambaye katika hostoria yake amewahi kubaguliwa kwa sababu ni mweusi, kwa zaidi ya miaka 20 amefanya harakati mbalimbali za kuwakomboa wanawake hasa wenye asili ya Afrika
Mbali na kuandika vitabu na kuandaa vipindi vya televisheni mwanamke huyo amekuwa akifanya makongamano mbalimbali ya kuwawezesha wanawake