VICTORIA SOUND KUZINDULIWA LEO
Bendi ya muziki wa dansi nchini Victoria Sound chini ya Muumini Mwinjuma inatarajiwa kuzinduliwa leo katika ukumbi wa Mango Garden ambapo mgeni rasmi atakuwa Abdisalam Khatibu aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha
Akizungumza Dar es Salaam kiongozi wa bendi hiyo Mwinjuma 'kocha wa dunia'alisema kuwa onyesho hilo pia litatambulisha wanamuziki wote wapya waliopo ndani ya bendi hiyo
Alisema onyesho hilo litasindikizwa na bendi ya muziki wa dansi ya Extra Bongo chini ya mkurugenzi wake Ally Choki pamoja na malikia wa mipasho Khadija Kopa