Google PlusRSS FeedEmail

WALTER AWEKA MIPANGO YA KUJIENDELEZA KIMUZIKI



MSHINDI wa kinyang'anyiro cha Epiq Bongo Star Seach, Walter Chilambo ameweka wazi kuwa ushindi pamoja na fedha alizozawadiwa ndiyo chanzo cha usumbufu anaoupata kutoka kwa baadhi ya wasichana

Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akielezea mipango aliyonayo kwa ajili ya kujiendeleza kimuziki huku akifuta dhana iliyopo kwa baadhi ya mashabiki kuwa washindi wa EBSS wanashindwa kumudu kwenye gemu la muziki

Alisema kuwa mmoja ya mikakati aliyokuwa nayo ni jinsi ya kupanga misingi bora huku akitumia busara na kuepuka vishawishi hususani kwa baadhi ya wasichana ambao wanaonekana kumtamani kwa sababu ya hela zilizotokana na ushindi wake, pia atazingatia misingi yote ya muziki  huku akitumia kipaji alichonacho na kuwa mbunifu katika kazi zake

Alisema kuwa amejipanga kufanya kazi hiyo kwa ubunifu wa hali ya juu ili kuondoa maneno ambayo yapo kwenye baadhi ya mashabiki kuwa washindi wa EBSS wanakuwa hawana vipaji na uwezo wa kudumu kwenye gemu la muziki

Aliongozea kuwa ili aweze kutimiza malengo yake hajaamua kutumia hela hiyo na bado yuko chini ya usimamizi kwa ajili ya kumuongoza nini afanya na kwa wakati gani

Walter ambaye ni mshindi wa EBSS 2012 ameweza kutoa single yake inayojulikana kwa jina la 'Siachi' iliyofanya na produza Ema theboy huku akiwa na mikakati ya kuachia nyimbo yake nyingine hivi karibuni

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging