Google PlusRSS FeedEmail

NOTORIOUS B.I.G'S CHILDHOOD HOME FOR SALE.

NOTORIOUS B.I.G
NYUMBA ya rapa maarufu hayati Christopher Wallace aka The Notorious B.I.G iliyopo jijini Brooklyn, Marekani imewekwa sokoni tayari kwa kuuzwa. Nyumba hiyo ambayo ina vyumba vitatu vya kulala na bafu moja inauzwa kwa kiasi cha dola 725,000 ikiwa kiasi kikubwa zaidi ikilinganishwa na mwaka 2004 ilipotangazwa kuuzwa kwa mara ya kwanza. Rapa alikuwa akiishi katika nyumba hiyo katika miaka ya zamani kabla hata hajapata jina la Biggie Smalls. 
Sebule ya nyumba hiyo.
Mmojawapo wa madalali wa nyumba hiyo hadhani kama historia ya Hip-Hop ya nyumba hiyo haiwezei kuathiri uuzwaji wake. Nyumba hiyo imekuwa ikitumika na wanandoa watu wazima lakini mara kwa mara imekuwa ikitembelewa na watalii wanaotaka kujua alikotokea rapa huyo ambaye alifariki dunia kwa kupigwa risasi. 

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging