REDD'S MISS IFM IKO JIKONI
Mashindano ya kumsaka Redd's Miss IFM 2013 yamefikia pazuri ambapo warembo 10 watapanda jukwaani Mei 25 mwaka huu kumsaka mrithi wa Fina Revocatus
Kinyang'anyiro hicho kinatarajia kufanyika katika hoteli ya JB Bellmonte maeneo ya posta mpya Dar es Salaam
Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa Redd's Miss IFM, Daniel Sarungi alisema mshindi wa taji hilo ataondoka na kitita cha sh. milioni moja
Meneja wa Redd's Original ambao ndiyo wadhamini wakuu wa Redd's Miss Tanzania Victoria Kimaro alisema wanajivunia kuwa sehemu ya udhamini na wanaamini warembo hao watafanya vizuri na kutwaa taji la Miss Tanzania