Kwa upande wa jumba la Diamond washiriki waliopigiwa kura nyingi kuingia kwenye Danger Zone na wenzao walikuwa ni Bolt wa Sierra Lione, Dillish wa Namibia na Hakeem wa Zimbabwe ambapo kama kawaida HOH huku nako pia alipata nafasi ya kumuokoa mmoja na kumbadilisha na mwingine. Katika chumba cha mahojiano HOH wa jumba la Diamond Betty kutoka Ethiopia alilipa kisasi kwa kumuokoa Bolt na kumuweka Feza ambaye ni mshiriki kutoka Tanzania katika Danger Zone. Kama utakumbuka Feza wiki iliyopita wakati akiwa HOH naye alimuokoa mmoja wa washiriki na kumuweka Betty.
Kwa maana hiyo washiriki Dillish, Hakeem na Feza ndio watakaopigiwa kura wiki hii, hivyo chonde chonde watanzania tujitahidi kumpigia kura mshiriki wetu Feza aendelee kubakia huko.
Kwa maana hiyo washiriki Dillish, Hakeem na Feza ndio watakaopigiwa kura wiki hii, hivyo chonde chonde watanzania tujitahidi kumpigia kura mshiriki wetu Feza aendelee kubakia huko.