ROSE NDAUKA ASHANGAZWA NA BAADHI YA WASANII KUTUMIA MIKOROGO
MSANII wa filamu nchini Rose Ndauka ashangazwa na baadhi ya wasanii wa filamu kujichubua ili kujiongezea urembo bila ya kujali kuharibu ngozi zao.
Mshangao huo umeibuka baada ya baadhi ya mashabiki wa filamu kushangazwa na muonekano wa baadhi ya wasanii kubadilika siku hadi siku.
Rose aliweka wazi kuwa chanzo cha kujichubua kwa baadhi ya wasanii hao ni kutaka kuongeza urembo katika muonekano wao huku wakiamini kuwa njia ya kuwa mrembo ni kujichubua.
Alisema kuwa kujichubua si njia sahihi ya kuongezea urembo bali ni njia ya kuendelea kujiharibu na kuonekana mzee hata kama umri wako ni mdogo.
"Mimi nawashangaa sana wanatafuta uzuri kwa njia ya kujichubua mimi sipaki mkorogo lakini bado niko vizuri na naonekana mrembo pia., hivyo kujichubua si kuongeza urembo waelewe hivyo" alisema Rose
Aliweka wazi kuwa baadhi ya wasanii wengi wanamuonekano tofauti na walivyoanza kazi yao ya sanaa, kutokana na mikorogo wanayoitumia.







