Google PlusRSS FeedEmail

YALIYOJIRI KWENYE SHINDANO LA BIG BROTHER AFRICA

        


Usiku wa jana Jumapili (June 2) haukuwa mzuri kwa wana Africa Mashariki hususani nchi za Kenya na Uganda baada ya team zinazowawakilisha katika Big Brother “The Chase” kupungua nguvu kutokana na wawakilishi Huddah Manroe wa Kenya na Denzel wa Uganda kupewa tiketi za kurejea makwao.
Mishale ya saa 1 za usiku kwa saa za Afrika Mashariki macho ya watazamaji wa nchi mbalimbali za Africa yalielekezwa katika Eviction show ya kwanza ya Big Brother Africa “The Chase” ambayo ndio ilikuwa na majibu ya nani watakaopewa tiketi za kurudi nyumbani usiku huo baada ya kudumu kwa wiki moja tu toka shindano hilo lianze wiki iliyopita (May 26).

Washiriki watano waliokuwa kikaangoni ni Huddah, Denzel, Selly, Natasha pamoja na Betty na kura za watazamaji zilifanikiwa kuwaokoa Selly, Natasha na Betty na kuwaacha Huddah na Denzel warudi nyumbani kuendelea na maisha yao ya kawaida.

Muda mfupi baada ya Huddah na Denzel kujua hatma ya uwepo wao katika jumba hilo lenye raha ya kila aina, Huddah ali tweet kwa mara ya kwanza toka tweet yake ya mwisho ya (June 19), na tweet yake ya kwanza jana ilikuwa “‏@HUDDAHMONROE.. And such is life….back to the hustle!” , iliyofuatiwa na tweet nyingine ya kuwashukuru fans wake wa Kenya na Africa kwa ujumla ‏”Thanks alot Kenya and the whole of Africa….You did ur part.God bless”.a

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging