Google PlusRSS FeedEmail

LAURYN HILL ATUPWA LUMANDE


MWIMBAJI  maarufu katika ulimwengu wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Lauryn Hill ambaye pia aliwahi kuwa katika kundi la Fugees pamoja na wasanii, Pras na Wyclif Jean, juzi alikwenda jela kuanza kutumikia kifungo cha miezi mitatu kwa kosa la kukwepa kulipa kodi ya mapato yake.

Mwanamuziki huyo, ambaye pia ni mama wa watoto watatu alikubali kosa mwaka jana kwa kushindwa kuweka rekodi za kodi ya mapato kwa zaidi ya dola za Marekani milioni 1.8 kutokea mwaka 2005 mpaka 2007.

Mshindi huyo wa tuzo za Grammy, alihukumiwa kwenda jela kwa miezi mitatu, ambapo atakuwa katika jela ya wanawake ya Danbury, iliyoko Connecticut nchini Marekani.

Hill ameshauza jumla ya zaidi ya nakala milioni 16 za albamu zake, lakini alipofika mbele ya jaji Mei, 2013 alisema; “ninaishi kawaida sana ukifananisha na kiasi cha pesa ninazozalisha kufaidisha wengine.

“Kuna mtu kapiga hesabu zake na kufikia kuwa nadaiwa dola milioni 600”.

“Niko mbele yako hapa najaribu kutafakari jinsi ya kulipa deni? Na kama haitoshi huo si utumwa sijui,” aliongeza.

Mwendesha mashtaka wa kesi hiyo alidai kuwa kiwango hicho cha fedha kwa kiasi kikubwa kimetokana na mapato ya mauzo ya muziki anaoimba Lauryn pamoja na mirabaha ya filamu aliyolipwa na kampuni mbalimbali katika kipindi cha mwaka 2005 mpaka 2008

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging