Google PlusRSS FeedEmail

VIDEO UJIO BARACK OBAMA

JINA KAMILI : Barack Hussein Obama AMEZALIWA : 4 Agosti 1961 ni rais wa 44 na rais wa sasa wa Marekani. ASILI YAKE : Yeye ni Mwafrika-Mwamerika wa kwanza kushika wadhifa huo, na pia mtu wa kwanza mwenye kuzaliwa Hawaii kuwa rais wa Marekani. Obama awali alihudumu kama Seneta mdogo kutoka jimbo la Illinois, tangu Januari 2005 hadi alipojiuzulu baada ya kushinda uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka 2008, mwezi wa Novemba. ELIMU YAKE : Obama alifuzu mwanzo kutoka katika chuo kikuu cha Columbia University, kisha akafuzu katika masomo ya kisheria kutoka katika kitivo cha masomo ya sheria kwenye chuo kikuu cha Harvard, ambako alikuwa rais wa jarida la Harvard Law Review. Alihudumu baadaye kama mwana-harakati wa mambo ya kijamii, kabla ya kuhitimu katika masomo ya kisheria. Hatimaye, alifanya kazi kama wakili wa haki za umma mjini Chicago, kisha akafunza sheria ya kikatiba katika Chuo Kikuu cha Chicago kuanzia 1992 hadi 2004. Obama alihudumu mihula mitatu katika Bunge la jimbo la Illinos (Illinois Senate) tangu 1997 hadi 2004. Baada ya kushindwa katika jitihada zake za kuchaguliwa katika Bunge Dogo la Marekani mwaka 2000, Obama alisimama kuchaguliwa katika Bunge La Maseneta La Marekani mwaka 2004. HISTORIA YA URAIS : Alishinda uchaguzi hapo Novemba 2004.Alitangaza kusimama kuchaguliwa kama rais wa Marekani mwezi Februari, mwaka 2007. Baada ya kampeni kali katika uteuzi wa chama cha Democratic Party dhidi ya Hillary Clinton, aliteuliwa kama muania-kiti cha urais kwenye tikiti ya chama hicho. Katika uchaguzi wa urais wa Marekani wa 2008, alimshinda John McCain, aliyekuwa ameteuliwa na chama cha Republican Party, na akaapishwa kama rais tarehe 20 Januari 2009. Tarehe 9 Oktoba 2009, Obama alituzwa kwa Tuzo ya Nobel ya Amani. ZIARA YA OBAMA NCHINI TANZANIA Dar es Salaam. Rais wa Marekani, Barack Obama amefanya ziara ya kihistoria nchini Tanzania, lakini ameacha mazuri na makovu. Ziara ya kiongozi huyo nchini aliyewasili juzi mchana ikiwa ni mwishoni mwa ziara yake barani Afrika baada ya kuzitembelea Senegal na Afrika Kusini, ilikuwa na furaha na karaha zake nchini. Rais Obama na ujumbe wake waliondoka jana saa 6:03 mchana kurejea Washington, Marekani kupitia Dakar, Senegal alipokuwa anatazamiwa kujaza mafuta kwenye ndege yake ya Air Force One. Ilikuwa ni ya furaha kwa Watanzania wote, lakini ilikuwa karaha kwa wakazi wengi wa Dar es Salaam. Ujio wa Obama, ambaye ana asili ya Afrika, ulisubiriwa kwa hamu na Watanzania wengi, wakitaka kumuona na kujua alichokuja kufanya. Furaha Moja ya mambo ya kufurahisha ni alipotaja vipaumbele vinne vya Marekani kwa Tanzania, ambavyo vinajumuisha miradi mbalimbali ya umeme, miundombinu ya barabara, maji na programu za vijana kwa lengo la kuongeza ajira. Katika eneo la miundombinu ya barabara licha ya kuwa tayari Marekani imeshasaidia ujenzi wa barabara ya Namtumbo-Songea, Mbinga, Horohoro na baadhi Kisiwa cha Pemba, itaendelea kutoa misaada zaidi. Mpango wake wa kuisaidia Tanzania sekta ya nishati kupitia mpango wa Power Afrika ambao utafikisha umeme vijijini, ni jambo la kufurahisha na lilipokelewa kwa shangwe. Mpango huo ambao utatumia dola 2.5 bilioni za Marekani (Sh4 trilioni) ni wa kati ya Marekani na nchi sita za Afrika; Tanzania, Ghana, Kenya, Liberia, Nigeria na Ethiopia. Karaha Pamoja na kuwa ziara hiyo ilikuwa ni ya furaha kwa Watanzania, pia ilikuwa na karaha ambazo zilisababisha mtiririko wa shughuli za kila siku kwa wakazi wa Dar es Salaam kukwama kutokana na ujio wake.Kufungwa kwa barabara ya Nyerere, Mandela, Sam Nujoma na Ali Hassan Mwinyi kulisababisha karaha kwa wananchi na kushindwa kwenda ofisini na pia kufanya biashara zao. Watu walishindwa kutoka nyumbani kuelekea katika shughuli zao kutokana na magari kutoruhusiwa kupita barabara alizokuwa akitumia rais huyo. Wafanyakazi wengi walishindwa kwenda ofisini kutokana na ratiba ya kiongozi huyo

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging