Google PlusRSS FeedEmail

GURUMO ASTAAFU MUZIKI, AKIWA MASIKINI

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini wa bendi ya Msondo Ngoma,  Muhidini Gurumo jana ametangaza kustaafu muziki rasmi kutokana na umri wake kuwa mkubwa.Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Gurumo alisema anastaafu shughuli za muziki huku maisha yake yakiwa duni kwani hana hata baiskeli.

Aliweka wazi kuwa umri wake kwa sasa umekuwa mkubwa ambapo alisema ameimba kwa kipindi cha miaka 53 akiwa jukwaani."Muziki ni kama asili yangu imefika wakati sasa nasema basi nawaachia vijana waweze kuendeleza muziki wetu" alisema Gurumo.Mzee huyo alianza kuimba muziki akiwa na umri wa miaka 20.

Aliweka wazi kuwa tangu aanze kuimba muziki hadi sasa ametoa kopi zaidi ya 60,000 ambazo hazijamfaidisha kimaisha hivyo ameamua kuunda kamati itakayokuwa inamsaidia katika kipindi hiki alichostaafu muziki.Kamati hiyo iliyoundwa na Gurumo ina wanamuziki na wakurugenzi wa bendi mbalimbali akiwemo Asha Baraka, Juma Mbizo, Saidi Mdoe, Waziri Ali na Saidi Kibiriki.

HISTORIA YA GURUMO.

Amezaliwa mkoa wa Pwani wilaya ya Kisarawe 1940. Elimu ya Msingi alisoma katika  Shule ya Pugu kuanzia darasa la kwanza mpaka la tatu, mwaka 1956, mjomba wake aliamua kumuamishia  Dar es Salaam ambako alisoma zaidi elimu ya dini 'Kuran', Mtaa wa Lindi, Ilala.Safari yake ya muziki ilianza rasmi mnamo mwaka 1967 alipojiunga na bendi ya Nuta kabla haijabadilishwa jina na kuitwa  Juwata, baadaye Ottu Jazz.

Mwaka 1978 aliamia Mlimani Park Orchestra na mwaka 1985 alijiunga na  Bendi ya Orchestra Safari Sound (OSS- Ndekule)  lakini siku zote maisha yake yamekuwa Msondo ambayo ndiyo bendi iliyopitia majina ya Nuta, Juwata na Ottu.

Tangu miaka ya 1960 kama ungethubutu kutamka humjui Gurumo, ungeonekana mshamba ambaye tasnia ya muziki umeipa kisogo,alikuwa staa mkubwa sana wa muziki kipindi hicho ingawa jina  lake limebaki juu kuanzia nyakati hizo mpaka sasa.

Ni kamanda hodari, aliyeifanya Bendi ya Msondo ‘Msondo Ngoma’ ipate heshima kubwa mpaka ikaitwa Baba ya Muziki Tanzania. Tungo zake nyingi ni lulu ambayo haitafutika kamwe. Kinachoumiza kwa sasa ni kuona Gurumo hawezi tena kusimama jukwaani.Mzee huyo ndiye aliyeivusha Msondo  kupitia majina ya Nuta, Juwata,  na Ottu, ikiwa inamilikiwa na Chama cha Wafanyakazi.

Itambulike kuwa yeye akiwa na wenzake kama marehemu Shaaban Mhoja Kishiwa  maarufu kama ‘TX Moshi William’, Saidi Mabera, marehemu Suleiman Mbwembwe, Othuman Momba, Joseph Maina na wengineo, ndiyo waliounganisha nguvu na kuimiliki, baada ya chama cha wafanyakazi kujiondoa katika uendeshaji wa bendi.


This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging