Google PlusRSS FeedEmail

WOLPER AIBUKA KIDEDEA WANAWAKE WENYE MVUTO BONGO MOVIE


WASANII wa filamu nchini Jacqueline Massawe 'Jaqline Wolper' pamoja na Hemedi Suleiman 'PHD' wameibuka washindi katika shindano la kumtafuta msanii wa filamu mwenye mvuto na anayependeza kutokana na mavazi anayoyavaa.

Wolpa amewabwaga wasanii wenzake wakike akiwemo Wema Sepetu ambaye walikuwa wanachuana huku PHD kumbwaga Yusuph Mlelwa  katika shindano hilo ambalo lilikuwa linaendeshwa na mtangazaji wa kipindi cha Take One kinachorushwa na kituo cha Clouds Tv.

Shindano hilo lilikuwa na lengo la kuwashindanisha wasanii wa filamu wa kike na wakiume anayeongoza kwa kuwa na muonekano wenye mvuto kuanzia mavazi, hadi anapoonekana kwenye macho ya watu.

Shindano hilo liliwashirikisha wananchi kwa kuwapigia kura wasanii hao wanaonekana wenye mvuto ambapo kwa upande wa wasichana ndipo Wolpa alipoibuka na kura nyingi, huku kwa upande wa kiume nafasi hiyo ikashikiriwa na PHD.

Akizungumza na jarida hili mara baada ya kutangazwa mshindi Wolper aliweka wazi kuwa hupenda kuvaa na kuonekana 'simple' wakati wote.

Alisema kuwa mbali na muonekano huo pia anaangalia mahali anapoenda na kuwa makini na kuchagua nguo inayoendana na mazingira ya sehemu hiyo na itakayoendana na yeye.

"Mimi navaa simple tu huwa sina makuu katika kuvaa ingawa mara nyingi pia ninaenda na fashion huku nikiangalia na mazingira siwezi nguo ya usiku nikavaa mchana" alisema Wolper.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging