Google PlusRSS FeedEmail

BABU SEYA APIGANIWA KORTINI

 
UPANDE wa utetezi umeiomba Mahakama ya Rufani Tanzania, kupitia marejeo ya rufaa iliyotolewa


 na mahakama hiyo katika kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamuziki mkongwe nchini Nguza Vikingi maarufu kama Babu seya kutoka na baadhi ya ushahidi uliotolewa na watoto haukuzingatia taratibu za sheria na kuitaka mahakama hiyo iondoe ushahidi huo na kuwaachia huru washitakiwa hao wawili.

Akiwasilisha hoja katika mahakama hiyo mbele ya jopo la Majaji watatu, ikiongozwa na  wakili wa wapinga rufaa, Mabere Marando alisema kuwa ipo haja ya mahakama kupitia marejeo ya rufaa hiyo na kuondoa ushahidi uliotolewa na baadhi ya wamashisi ambao walikuwa ni watoto kwa kuwa hawakuapishwa kabla ya kutoa ushahidi.

Alidai kuwa anaomba mahakama ibadili msimamo kwamba ushahidi wa mtoto mdogo usipofuata utaratibu uamuzi utakaotolewa ni batili.

Alisema kuwa kesi ya Nguza haikufuata utaratibu wa kisheria wakati wa kuwahoji watoto na kutaka ushahidi huo uondolewe kwenye kumbukumbu ya mahakama na kuona kwamba washitakiwa wawe huru.

Alisema kuwa mbali na ushahidi wa watoto kutozingatia utaratibu, pia katika sheria ya ushahidi kifungu cha 120 kinaeleza kwamba kama kuna tukio limetokea na mtu akaonekana kutajwa sana kwenye ushahidi upande wa mashitaka ni lazima mtu huyo aitwe ili aeleze.

Alisema kuwa lakini katika kesi ya Nguza ushahidi uliotolewa unaonyesha kwamba kwenye nyumba ambayo inadaiwa vitendo vya unajisi watoto vilifanyika ukitoka kwa nje ya nyumba hiyo utakutana na duka la Mangi a,bapo inadaiwa kuwa kama kuna kitu kinaendelea kwenye nyumba hiyo Mangi anaona lakini Mangi hakuitwa.

Alidai kuwa Mangi alikuwa shahidi muhimu sana kwenye kesi hiyo kwa kuwa anadaiwa yupo karibu sana na nyumba hiyo.

Alidai kuwa katika ukurasa wa 38 wa hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo, majaji walitamka kwamna shahidi 13 aliieleza mahakama kuwa mtu anaweza kuingia nyumba ya Nguza bila mtu yoyote kuona wakati ushahidi mwingine unaonyesha kwamba duka la Mangi lipo karibu na nyumba hiyo ambapo kila kitakachofanyika ndani kinaonekana.

Alisema pia katika kesi hiyo shahidi mwingine ambaye ndiye aliyekuwa akiwapeleka watoto kwenye nyumba nya Nguza pia hakuitwa,

Alidai kuwa baadhi ya mashahidi muhimu kutoitwa ili kuisaidia mahakama imesababisha mahakama kutotoa uamuzi wa haki. Alisema pia mahakama haikuona umuhimu wa ushahidi uliotolewa na upande wa utetezi hivyo kama mahakama ingetilia umuhimu utetezi huo ingejiridhisha.

Alisema ushahidi wa utetezi ulionyesha kwamba wanamuziki wa bendi ya Nguza walikuwa wakipiga magita kwenye nyumba ya Nguza kila siku kuazia jumatatu hadi juma piliuieleza mahakama kilichotokea ndio maana kuwepo kwa makosa katika ushahidi na kutaka baadhi ya usha

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging