Google PlusRSS FeedEmail

GAGA ATOSWA NA MPENZI WAKE



MSANII wa kike kutoka Marekani ambaye haishi vituko Lady Gaga imebainika kuwa huandika nyimbo zake akiwa anaoga na huota nguo mpya za kuvaa akiwa amelala hali inayomfanya kuwa bize kila wakati na matokeo anakosa muda wa kukaa na mpenzi wake hali inayopelekea mahusiano yao kuwa na mgogoro.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun limedai kuwa Gaga ameachwa na mpenzi wake ambaye pia ni muigizaji anayejulikana kwa jina la Taylor Kinney kutokana na kuwa na kazi nyingi hadi kukosa muda wa kukaa pamoja.

Gazeti hilo lilidai kuwa uhusiano wao umekuwa matatani kwa miezi kadhaa kutokana na Lady Gaga kuwa na kazi nyingi pamoja na kuangaika na kujionesha kila siku .

Chanzo kimoja kimeeleza gazeti hilo kuwa Tayrlor kuwa alimuweka wazi Gaga kuwa hawezi kuwa na uhusiano na staa huyo ambaye anamuda mfupi wa kukaa naye huku akiwa amezungukwa na wasaidizi kibao pamoja na walinzi .

Imebainika kuwa wapenzi hao wanamuda wa siku mmoja tu ndani ya mwezi mzima wa kuwa pamoja hali ambayo imemfanya Kinney kuchanganyikiwa kwa kuwa pekee yake mara nyingi.

Wakati huo huo Gaga ameonesha kituko baada ya kuweka meno ya bandia yaliyotokeza nje kwenye tuzo za Youtube zilizofanyika Jumapili hii huko New York City Marekani.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging